Kuwezesha Biashara Kufanya Maamuzi Kupitia Takwimu Zinazotolea Na Mfumo
Kutosikia sauti za mteja ni kikwazo kikubwa kwa ukuaji wa biashara nyingi. TumaMaoni inadhamira ya kutatua tatizo hilo.
Tunaamini kwamba kila maoni ya mteja ni fursa ya dhahabu ya kuboresha huduma. Mfumo wetu unatoa njia rahisi, isiyo na gharama kubwa, na ya papo kwa papo kwa wafanyabiashara kukusanya na kutathmini maoni.
Lengo letu ni kuwawezesha wajasiriamali Tanzania kutoka migahawa midogo hadi makampuni makubwa kufanya maamuzi yanayotokana na data halisi.
Hatua Rahisi za Kuanza
Mchakato mzima umebuniwa kuwa rahisi na wa haraka kwa wewe na wateja wako.
Jisajili
Fungua akaunti ya biashara yako kwa sekunde chache. Ni bure kuanza.
Pata QR Code
Mfumo utakupa QR Code maalum kwa ajili ya biashara au duka lako ikiwa na jina na logo ya duka lako.
Kusanya Maoni
Print na Weka QR dukani. Wateja wataichanganua na kutuma maoni bila kuacha namba ya simu.
Chambua Data
Ingia kwenye dashibodi yako kuona ripoti za kina na maeneo ya kuboresha.
Vipengele vya Kipekee
Haraka na Rahisi
Hakuna kupakua app kwa wateja. Scan tu na utoe maoni. Hii inaongeza idadi ya maoni unayopata.
Maoni ya Siri (Anonymous)
Wateja huwa wawazi zaidi wanapojua hawajulikani. Tunalinda utambulisho wao ili upate ukweli mtupu.
Dashibodi Hai
Fuatilia maoni yanapoingia papo kwa hapo. Pata arifa na uchukue hatua kabla tatizo halijakuwa kubwa.
Ripoti Zinazopakulika
Pakua ripoti za kila wiki au mwezi katika format ya PDF au Excel kwa ajili ya vikao vya uongozi.
Lugha Mbili
Mfumo wetu unapatikana kwa Kiswahili na Kiingereza, kuwafikia wateja wa aina zote.
Msaada wa Karibu
Timu yetu ipo tayari kukusaidia wakati wote kuhakikisha mfumo unafanya kazi kwa ufanisi.
Uko Tayari Kuboresha Biashara Yako?
Jiunge na mamia ya wafanyabiashara wanaoamini TumaMaoni.
Anza Bure Leo